Na Daudi Manongi-DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa hali ya
upatikanaji wa Dawa nchini imeimarika na kufikia asilimia 83.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Wizara hiyo Mhe.Khamis Kigwagalla alipokuwa akijibu Hoja mbalimbali za
Wabunge leo Mjini Dodoma.
“Moja ya vipaumbele vya Serikali
ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli ni
kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya
vya umma nchini”Alisema Mhe.Kigwangalla.
Amesema kuwa katika kutekeleza
azma hii Serikali ilichukua juhudi za makusudi kwa kuongeza bajeti ya
dawa kutoka bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/16 hadi kufikia
bilioni 251,500,000,000 katika mwaka wa fedha 2016/17.
Aidha hadi kufikia Mwezi April
2017 Jumla ya Bilioni 112 zilikwisha kutolewa na kupelekwa Bohari ya
Dawa ili kuviwezesha vituo vya kutolewa huduma za Afya vya Umma kupata
mahitaji yake ya Dawa,Vifaa,Vifaa tiba na Vitendanishi.
Kufuatia Ongezeko ilo la fedha kumbukumbu zinaonyesha kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini imeimarika sana.
“Hadi kufikia tarehe 15 Januari
2017,Mkoa wa Kagera pekee umepokea kiasi cha bilioni 4,150,767,216
kupitia fungu 52 kwa ajili ya kununulia dawa,vifaa,vifaa tiba na
vitendanishi.”Aliongeza Mhe.Kingwangalla.
Post a Comment