Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

MAMA SAMIA AWATAKA WAKUNGA KUFANYA KAZI KWA BIDII

ZA 3
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia  kwenye
kilele cha siku ya Wakunga Duniani ambapo Kitaifa imefanyika mjini
Dodoma. 


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Samia akihutubia Wakunga kwenye kilele cha Sherehe za Siku ya Wakunga Duniani iliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma kwenye ukumbi wa Julius K. Nyerere Chuo cha Mipango.

Wakunga wakirekodi hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa zimefanyika mjini Dodoma.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia Wakunga waliojitokeza kwa wingi kwenye kilele cha Siku ya Wakunga Duniani ambayo Kitaifa imefanyika mkoani Dodoma na mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
                                                   ……………………………………………………. 
Normal
0
false
false
false
EN-GB
X-NONE
X-NONE
MicrosoftInternetExplorer4
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0cm 5.4pt 0cm 5.4pt;
mso-para-margin-top:0cm;
mso-para-margin-right:0cm;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0cm;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}

     Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameziagiza Halmashauri zote nchini zihakikishe zinajenga nyumba kwa ajili ya watumishi wa
afya hasa maeneo ya vijijini na kipaumbele kitolewe kwa wakunga ambao mara
nyingi ndio wanatoa huduma za dharura kwa wanawake wajawazito na watoto.

Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo mjini Dodoma katika kilele cha
maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani sherehe ambazo zimehudhuriwa na Mamia ya
wakunga kutoka mikoa mbalimbali nchini.
 

Makamu wa
Rais amesema kuwa halmashauri zikijenga nyumba karibu na vituo vya kutolewa
huduma za afya zitasaidia kupunguza matatizo ya mama na watoto wanaotaka kupata
huduma za dharura ikilinganishwa na hali ilivyo sasa ambapo baadhi ya watumishi
wa afya hasa wakunga wanakaa mbali na maeneo yao ya kazi hivyo utoaji wa huduma
za dharura kuwa duni.

Makamu wa
Rais amewahimiza Wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia ujenzi huo kikamilifu kama
walivyoshughulikia matatizo ya madawati katika maeneo yao ili kuhakikisha Taifa
linafikia malengo yake ya kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi
nchini
.
 

Kuhusu
changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchini, Makamu wa Rais amewahakikishia wakunga na
watumishi wengine wa sekta ya afya nchini kuwa Serikali inaendelea kufanyia
kazi changamoto hizo ikiwemo uboreshaji wa maslahi kwa watumishi wa kada hiyo
pamoja na kuongeza maradufu vifaa tiba,dawa na vitendanishi ili kuhakikisha
wananchi kote nchini wanapata huduma bora za afya.

Amesema mpaka
sasa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya afya nchini ni imefikia asilimia 83
hadi kufikia mwishoni mwa Marchi 2017.
 

Makamu wa
Rais pia amewahimiza wakunga kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia maadili
na waache tabia ya kutoa lugha mbaya kwa wanawake wajawazito na wakunga
watakaobainika kufanya vitendo hivyo wachukuliwe hatua kali ili kukomesha tabia
hiyo.
 

Kwa
upande wake, Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amemhakikishia
Makamu wa Rais kuwa Wizara yake itaendelea kusimamia ipasavyo utoaji bora za
afya kwa wananchi pamoja na kusimamia maadili kwa watumishi wa sekta ya afya
kote nchini.

Amesema
anaimani kubwa kuwa baada ya Serikali kuiongezea Wizara ya Afya bajeti kutoka
bilioni zaidi ya 700 katika mwaka wa fedha za 2016/2017 hadi Trilioni Moja kwa
mwaka wa fedha 2017/2018 inaonyesha wazi dhamira ya dhati ya Serikali ya
kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa kiwango hali ya juu nchini
ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Kauli
mbinu ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga mwaka huu ni Wakunga,Akina mama
na Familia ni washirika wa Kudumu.
(Midwives,Women and Families
Partners)


KAWAIDAA
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget