RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya wiki moja, hiyo ni kulingana na taarifa katika mtandao wa kijamii kutoka kwa mmoja wa wasaidizi wake.
Mkanda mfupi wa video, unamuonyesha Buhari akizungumza na watu, baada ya kutoka msikitini kwa swalah ya Ijumaa katika Ikulu ya Rais.
Kumekuwepo na tetesi kuhusiana na afya ya Rais huyo, kwani hajaonekana hadharani tangu aliporejea Nigeria kutoka kwa ziara ya matibabu ya wiki saba nchini Uingereza, alipokwenda kutibiwa ugonjwa ambao bado haujajulikana.
Pia hajahudhuria mikutano mitatu ya baraza la mawaziri, na hakuhudhuria maombi ya ijumaa msikitini juma lililopita.
Lakini washauri wake wanasema kwamba, alikuwa akipumzika huku akifanya kazi akiwa nyumbani.
Chanzo BBC News
Post a Comment