Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini
ya miaka 17 “Serengeti Boys” imepata ushindi wa tatu mfululizo tangu
iondoke nchini kwenda kuweka kambi maalum kwa ajili ya maandalizi
kujiandaa na mashindano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka 17
itakayoanza mwezi Mei 14, 2017.
Serengeti Boys wameifunga timu ya taifa ya vijana ya
Cameroon kwa goli 1-0 lililofungwa na Ally Ng’anzi kipindi cha kwanza
katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Huu ni mchezo wa tatu Serengeti inashinda mfululizo,
ilishinda mechi mbili za kirafiki dhidi ya Gabon zilizochezwa nchini
Morocco ambako Serengeti ilikua imeweka kambi kabla ya kwenda Cameroon.
Baada ya kumaliza kambi nchini Cameroon itaondoka na
kuelekea moja kwa moja Gabon ambako zitafanyika fainali za michuano hiyo
ya vijana itakayoshirikisha mataifa nane.
Mtazamo juu ya Serengeti Boys ni kuendelea kuwa nayo na
kuifanya iwe ni timu ya taifa kwa miaka ya mbeleni kikubwa ni kutowatupa
vijana hawa pindi warudipo kutoka mashindanoni na watafutiwe timu
ambazo kwa mfumo yakini kabisa wawe wanacheza ili kuendelea kujifunza
kadri siku zinavyokwenda.
Post a Comment