Klabu ya Simba
imesema kuwa, itapeleka malalamiko yao katika Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa) kutokana na kudhulumiwa mchezaji wao, Mbaraka Yusuph
anayekipiga kwenye kikosi cha Kagera Sugar.
Rais wa Simba, Evans
Aveva, ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari huku akiwa na
leseni mkononi ya mchezaji huyo inayoonesha mwanzoni mwa msimu huu
walimsajili ili aitumikie Simba, lakini wakashangaa anaichezea Kagera
Sugar.
“Mbaraka Yusuph jina
lake pamoja na majina yote ya wachezaji wetu wa msimu huu
tuliyawasilisha TFF na tukapewa leseni zao wote kuidhinisha kwamba
tuwatumie msimu huu. Cha kushangaza tukaona anaichezea Kagera Sugar.
“Malalamiko yetu
yapo TFF kwa muda mrefu lakini mpaka sasa hatujapewa majibu yoyote, sasa
tunaamua kwenda Fifa kudai haki yetu juu ya mchezaji huyu ambaye leseni
yake inayoonyesha ni mchezaji wetu tunayo mpaka sasa,” alisema Aveva.
Post a Comment