Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia
Mjema amewaagiza madereva wa daladala na bajaji kuhakikisha vyombo vyao
vya usafiri vinakuwa na kikapu cha kuwekea taka, vinginevyo watatozwa
faini ya uchafuzi wa mazingira.
Akizungumza leo jijini Dar es
Salaam katika kufanya kwa vitendo kampeni ya usafi ya kila jumamosi ya
mwisho wa mwezi DC Mjema alitembelea kituo cha daladala cha stesheni na
kukuta magari mengi ya abiria hayana vikapo vya taka, ambapo wameyatoza
takribani magari saba kiasi cha shilingi 50000 kwa kila moja katika
eneo hilo.
Huku kwa upande wa madereva wa
bajaji wanaopaki eneo la Soko la Samaki Feri wamepewa onyo na kuombwa
kufanya hivyo mara moja kabla hawajachuliwa hatua na mamlaka husika ya
Halmashauri hiyo ya Ilala.
Katika hatua nyingine DC Mjema
amewataka wafanyabishara wadogo wanaopanga bidhaa zao kandokando ya
barabara iliyopo jirani na soko la samaki Feri kujiandikisha kwa afisa
mtendaji na kuondoka eneo hilo mara moja, huku Halmashauri hiyo
itawapangia maeneo ya biashara ndani ya soko hilo la samaki la Feri.
Post a Comment