Taasisi ya Tafiti za
Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo
nchini kuijadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambao
unaelekea kuisha.
Akizungumza katika mkutano huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema mdahalo huo ni
sehemu ya shughuli ambazo zinafanywa na ESRF ili kutazama ni njinsi gani
Taasisi inaweza kuisaidia Serikali kuweka mipango thabiti kwa ajili ya
maendeleo ya nchi.
Dkt. Kida alisema mdahalo huo
ulihusu bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia kwa kuangalia utekelezaji wa bajeti zilizopitishwa
kwa mwaka wa fedha 2016/2017, changamoto zilizopo na nini kifanyike
katika bajeti ya 2017/2018.
“ESRF imekuwa ikishirikiana na
wadau ili kuangalia ni jinsi gani tunaweza kusaidia mchakato wa
maendeleo wa nchi yetu kwa njia ya utafiti mbalimbali, uchambuzi na
utayarishaji wa sera na kuongeza wadau uwezo kupitia mafunzo mbalimbali.
“Kama jinsi mnavyojua nchi yetu
imekuwa na mipango ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia bajeti kwa
kuangalia mambo yenye umuhimu kwa Taifa, bajeti imekuwa ikipangwa kila
mwaka kwa kuzingatia maeneo ya kuyapa kipaumbele ili kuleta maendeleo
kwa nchi.” alisema Dkt. Kida.
Kwa upande wa mtoa taarifa ya
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Joviter Katabaro (Mkufunzi
katika, shule ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) alisema pamoja na
serikali kutoa elimu bure katika ngazi fulani ya elimu nchini lakini
bado kuna changamoto mbalimbali katika elimu ambazo zinahitaji
kutafutiwa ufumbuzi katika bajeti ya 2017/2018.
“Pamoja na jitihada kubwa ya
Serikali katika elimu bado kuna upungufu wa majengo 10,000 ya shule
nchini kitoke, kuna upungufu wa maktaba 15,000, vyoo bado havitoshi,”
alisema Dk. Katabaro.
Kwa upande wake, Prof. Haidari
Amani (Mtafiti Mshirki mwandamizi ESRF) ambaye alitoa taarifa kuhusu
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi alisema pamoja na sekta ya kilimo kuwa
na changamoto ambazo zinajitokeza serikali inatakiwa iweke mfumo mzuri
kuanzia wakulima wadogo ili waweze kunufaika na kilimo ambacho
wanakifanya.
KAWAIDA
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF) imewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini
kuijadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambao unaelekea
kuisha.
Akizungumza katika mkutano huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema mdahalo huo ni
sehemu ya shughuli ambazo zinafanywa na ESRF ili kutazama ni njinsi gani
Taasisi inaweza kuisaidia Serikali kuweka mipango thabiti kwa ajili ya
maendeleo ya nchi.
Dkt. Kida alisema mdahalo huo
ulihusu bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia kwa kuangalia utekelezaji wa bajeti zilizopitishwa
kwa mwaka wa fedha 2016/2017, changamoto zilizopo na nini kifanyike
katika bajeti ya 2017/2018.
Post a Comment