Rais
John Magufuli leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Siku
ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kitaifa. Kwa mujibu wa Shirikisho la
Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), sherehe hizo zitafanyika
kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).
Rais
Magufuli aliwasili mjini Moshi juzi akitokea mkoani Dodoma na jana
alishiriki Ibada za Jumapili katika makanisa mawili tofauti, na leo
anatarajiwa kuongoza maelfu ya wakazi wa Moshi na miji jirani katika
kilele cha sherehe hizo za Mei Mosi, huku wafanyakazi wakililia hali
bora makazini.
Akizungumza
wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Tucta, Yahaya Msigwa alisema, “Tayari
tumemwandikia Rais Dk Magufuli kumuomba awe mgeni rasmi, kimsingi
sherehe zote kitaifa mgeni rasmi ni yeye...tunazo ajenda za kumpa Rais,
lakini moja ya mambo ambayo ni kero ni hili la mikataba ya hali bora
kazini, wafanyakazi wengi wanafanya kazi kama vibarua na hawajui haki
zao.”
Kwa
mujibu wa takwimu za Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania
(TUCTA), Taifa lilipaswa kuwa na waajiriwa milioni 3.7 katika sekta
iliyo rasmi, lakini waliopo ni 650,000 pekee hali inayoashiria kutokuwa
na mikataba.
Alitolea
mfano wa watumishi wa mashambani pekee nchini Kenya ni zaidi ya 700,000
na Afrika Kusini ni zaidi ya milioni moja na kwamba ipo haja kwa
waajiri Tanzania kutafakari upya suala la maslahi ya wafanyakazi wao na
rais anapaswa kulisemea hilo.
Post a Comment