Mbunge wa viti malum
mkoani Pwani, Subira Mgalu mwenye kitambaa kichwani akitembelea bidhaa
mbalimbali zaywajasiriamali kwenye uzinduzi wa umoja wa kikundi cha
Pwani Generation Queens. (Mwamvua Mwinyi)
Mbunge viti maalum
mkoani Pwani, Subira Mgalu akizungumza wakati wa uzinduzi wa umoja wa
kikundi cha Pwani Generation Queens, uliofanyika Triple J, Pichandege
Kibaha. (picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Mbunge wa viti
maalum mkoani Pwani Subira Mgalu, amewataka wanawake kuacha ubinafsi
/kujibweteka,badala yake wathubutu kujenga umoja na kuchapa kazi ili
kujiinua kiuchumi.
Aidha amekemea tabia ya kusemana, fitna na majungu kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha vikundi vingi kuvunjika .
Akizindua umoja wa
kikundi cha wanawake wajasiriamali (Pwani generation queens),Subira
alisema, wanawake ni jeshi kubwa endapo wakijidhatiti kwa kutumia fursa
za maendeleo watapiga hatua zaidi.
Alieleza
kwamba, zipo fursa mbalimbali zinazoweza kuwasaidia wanawake lakini
kama wataendelea kujiweka peke, fursa hizo hazitoweza kuwafikia mmoja
mmoja.
Subira alibainisha fursa mojawapo ni sanjali na kutumia taasisi ya uwezeshaji chini ya serikali -baraza la uwezeshaji la taifa.
“Wengi hawalifahamu ,lakini taasisi hiyo inatoa
udhamini kwa umoja wa vikundi,na kudhamini kukopa kwenye taasisi za
kifedha ikiwemo Tanzania Posta Bank, bank ya Wanawake nchini na NMB.
“alisema.
Mbunge huyo alielezea, taasisi hizo zinatoza asilimia nafuu ambapo Tanzania posta bank wanachaji asilimia tatu.
“Napongeza serikali kwa namna waziri wa ofisi ya
waziri mkuu kuzileta pamoja taasisi za uwezeshaji, sisi wawakilishi
kazi yetu kuzifuatilia, kuziletea mrejesho na kutoa elimu kwa vikundi
mbalimbali vya ujasiriamali viweze kuungana kwa kuandaa katiba ili
vipate fursa “alisema.
Kwa mujibu wa Subira, tayari bank kuu imepunguza
riba ambayo zinatoa taasisi nyingine za kifedha hivyo anaamini taasisi
hizo zitapunguza riba.
Subira
aliiomba serikali, kama ilivyochukua hatua kupitia bank kuu kuingilia
kwa kupanda kwa riba kwenye taasisi za kifedha ambazo zina hisa zake
ikiwemo bank ya wanawake.
Hata hivyo alisema,
amekuwa champion na muumini wa kusisitiza halmashauri kutenga asilimia
tano za wanawake na asilimia tano kwa vijana.
Aliwataka wanawake
waache kujitenga bali waungane ili waweze kunufaika na fedha za
halmashauri, taasisi zisizo za kiserikali na baraza la uwezeshaji.
Awali akizindua kikundi cha Pwani Generation Queens, alijiunga na kikundi hicho kwa kuchangia sh. 100,000 .
Subira aliuomba umoja huo waache tofauti zao, wapendane ili wawe mfano katika mkoa wa Pwani na mikoa mingine.
Nae mwenyekiti wa
kikundi cha malkia Pwani, Betty Msimbe, alisema kikundi hicho ni
kichanga kikiwa na wanachama 100 na kinaongozwa na katiba .
Alisema wanachama wake ni kuanzia miaka 18 na kuendelea wakiwa ni wakazi wa maeneo ya wilaya ya Kibaha,Kisarawe na Ubungo .
Betty alisema, lengo la kikundi ni kushirikiana katika mipango ya kimaendeleo, shida na raha na kuwezeshana.
Nao wanachama wa
kikundi, Rehema Kawambwa, Zarina Zenzele walisema endapo watashirikiana
wanaamini nia na malengo ya kikundi yatafikiwa.
Waliomba serikali na taasisi mbalimbali za kijamii kuwaunga mkono ili waweze kuwezeshwa na kupiga hatua kiuchumi.
Post a Comment