KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki
na Kati, Azam FC, inatarajia kuondoka nchini kesho Jumatano alfajiri,
tayari kabisa kuelekea Rwanda kukipiga na Rayon Sports Jumamosi ijayo.
Kikosi cha Azam FC hivi sasa kipo
kwenye maandalizi makali kujiandaa na msimu ujao, ambapo itacheza na
Rayon katika mchezo maalum wa kusherehesha ubingwa wa Ligi Kuu Rwanda
iliyoutwaa timu hiyo.
Mara baada ya mchezo huo, kikosi hicho kitaanza safari ya kurejea nchini Jumapili ijayo.
Mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi
na Ngao ya Jamii msimu uliopita, wanaendelea na mazoezi huku ikiwakosa
wachezaji wake kadhaa Nahodha Msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, beki Erasto
Nyoni, kiungo Salmin Hoza na washambuliaji Mbaraka Yusuph na Shaaban
Idd, ambao wako timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Nyota hao wako na Stars
inayoshiriki michuano ya Kombe la COSAFA inayoendelea nchini Afrika
Kusini, ambapo timu hiyo ikiwa imetinga hatua ya nusu fainali na
ikitarajiwa kucheza na Zambia kesho.
Wengine ambao bado hawajawasili ni
mabeki Yakubu Mohammed, Daniel Amoah, winga Eneock Atta Agyei (Ghana),
kiungo Mcameroon Stephan Kingue na mshambuliaji Wazir Junior,
aliyesajiliwa akitokea Toto Africans ya Mwanza.
Post a Comment