Mpogolo ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la benki ya NMB Tanzania kwenye maonesho ya Saba Saba ambapo alipata nafasi ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali ambazo zinatolewa na benki hiyo kubwa nchini.
Alisema kuwa akaunti hiyo ni nzuri sababu inawagusa watu wa hali ya chini na maisha ya kati, kundi ambalo linajumuisha sehemu kubwa ya Watanzania na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo kufungua akaunti ya Fanikiwa ili waweze lupata huduma mbalimbali zinapotaikana kwenye akaunti hiyo.
“Inalenga kuwasaidia watu wa kaiwada kukuza mitaji na kuendeleza kipato chao, mtu anapopata nafasi ya kupata mkopo maana anaweza kuongeza kipato cha familia na ndivyo uchumi wa taifa unavyoweza kujengwa,
“Mimi niwapongeze NMB kwa kuanzisha Fanikiwa Account na niwahamasihe Watanzania watumie fursa hii kuweza kuongeza kipato kwa ajili ya maisha yao na waweze kuongeza kipato,” alisema Mpogolo.
Aidha Mpogolo alizungumza kuhusu baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakihofia kuchukua mikopo kwenye mabenki ili waweze kuongeza kipato, “Ni jukumu la kila mtu kumuhamasiaha mwenzake aone benki ni mahali anapoweza kupata fursa za kujikomboa kiuchumi, kuendeleza ustawi wake mambo kama haya zamani hayakuwepo ambayo yanagusa watu wa hali ya chini,
“Mimi jambo ambalo limenigusa ni kuanzisha akaunti ambayo inagusa watu wa kipato cha chini, naona kwamba Benki ya NMB inakwenda kuwa mkombozi wa watu wanyonge kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais na serikali yake ya kuona wananachi wa kawaida na wao wanaboresha uchumi wao.”
Post a Comment