Makampuni ya Tanzania ya uwakala wa
usambazaji wa bidhaa za kutoka nje ya nchi, wameshauriwa kuyashawishi
makampuni ya nje kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hapa hapa nchini.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi ametoa ushauri huo jijini Dar es
salaam wakati akitembelea mabanda ya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara,
na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono kwa
vitendo jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kutaka kuigeuza Tanzania
kuwa nchi ya viwanda.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akielekea
kukagua baadhi ya matrekta katika banda la Kampuni ya Agricom
akiambatana na Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric
Mwidunda (kulia kwa Dr.Mengi) alipotembelea kwenye maonesho ya 41 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya
Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam.
Akifuatana na Mkurugenzi wa TPSF Bw.
Louis Accaro, Afisa Biashara wa Tan-Trade Bw. Mohamed Mkadara, na
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wajasiriamali Bi. Jacquiline Maleko, Dr
Mengi ametembelea mabanda mbalimbali, yakiwemo yaliyopo chini ya
mwamvuli wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda, na Kilimo – TCCIA,
Mfuko wa Fursa sawa kwa wote-EOTF, na Banda la Kampuni ya Agricom,
ambayo Mkurugenzi wake Mtendaji Bi. Angelina Ngalula alielezea jinsi
ilivyojipanga kusambaza zana za kisasa za kilimo ili kumpunguzia mkulima
gharama za uzalishaji.
Katika majumuisho yake Dr Mengi
alishauri Tan-Trade na TPSF washirikiane katika kuangalia namna ya
kuboresha zaidi maonyesho hayo, hususan katika kuboresha mabanda ya
maonyesho ili yalingane na hadhi halisi ya kimataifa.
Meneja
Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kushoto) akitoa
maelezo kuhusu ubora wa matrekta hayo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kushoto)
alipotembelea kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere
(Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Agricom, Bi. Angelina Ngalula (kushoto)
akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania –
TPSF Dr. Reginald Mengi alipotembelea banda la kampuni hiyo kujionea
huduma zao kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea
katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba)
barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa miradi na mshauri wa Maisha Finance Ltd, ambao ni wakopeshaji wa
zana zote za kilimo yakiwemo Matrekta ya kampuni ya Agricom, Erasmus
Erneus akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja, Apollos Rweikiza
aliyetembelea banda la Agricom katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya
Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K
Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akiwa
ameambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania
(TWCC) Jacqueline Maleko (wa pili kushoto) alipowasili kwenye banda la
TWCC yanakoendelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika Uwanja
wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya
Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Fedha, Masoko na Usafirishaji wa C.E Holdings Ltd, wauzaji wa vito
vya Afrika, Maria Pagama akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya
Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la
TWCC kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika
Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Picha
juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF
Dr Reginald Mengi akifurahia jambo na wanawake wafanyabiashara kwenye
banda la TWCC katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba
Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha ya juu kulia ni
Noreed Mawalla wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC).
Mkurugenzi
wa Tanfood and Spice Co. Investment watengenezaji wa bidhaa za kutunza
ngozi zinazotokana na mimea, Bi. Rona akitoa maelezo ya bidhaa halisi za
kutunza ngozi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania –
TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la TWCC kwenye maonesho ya 41
ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya
Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitoa
maelekezo kwa Noreed Mawalla wa TWCC (katikati) wakati akitembelea banda
la Chama cha wafanyabiashara wanawake kwenye maonesho ya 41 ya Biashara
ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya maonesho ya Biashara wa Mwl J.K
Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC)
Jacqueline Maleko.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi
akitazama bidhaa mbalimbali katika banda la Chama Cha Wanawake
Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) lililopo katika maonesho ya 41 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimuongoza
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald
Mengi mara baada ya kuwasili katika banda la EOTF kwenye maonesho ya 41
ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Joane Art Craft, Culture
& Desigin, Bi. Joane Baigana (kulia) alipotembelea banda la EOTF
kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika
Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi
akitazama kazi mbalimbali za wakinamama wajasiriamali kwenye banda la
EOTF katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Uwanja
wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya
Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa
kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi
akisalimiana na wanawake wajasiriamali wanaofadhiliwa na EOTF akiendelea
kutembelea wajasiriamali katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere
(Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Anayemuongoza ni
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akisaini
kitabu cha wageni katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
lililopo ndani ya banda la EOTF yanakoendelea maonesho ya 41 ya Biashara
ya Kimataifa katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere
(Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi
akitazama moja ya vitabu katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu lililopo ndani ya banda la EOTF. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa
Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akipata
maelezo ya huduma mbalimbali za mikopo riba nafuu kwa wanawake kutoka
kwa Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanzania Women’s Bank, Renita Michael
(kulia) ndani banda la EOTF wakati alipotembelea maonesho ya 41 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa maonesho ya
Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF),
Mama Anna Mkapa na Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake
Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko.
Post a Comment