NA CHRISTINA MWAGALA ,OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema
watanzania hawajafikia hatua ya kubaguana kwa kiitikadi ya vyama, Dini,
Kabila badala yake wote wanapaswa kutangaza hali ya Umoja, Upendo na
Mshikamano katika nchi yao.
Meya Mwita alitoa kauli hiyo jijini hapa jana, wakati wa harambee
ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa la kisasa la Tanzania Assemblies Of
God (TAG) lililopo Kivule ,Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini hapa
ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa watanzania wanapaswa kuwa
wamoja ili nchi iendelee kuwa na amani.
Alisema yapo mambo mbalimbali ambayo yanajitokeza ndani ya nchi
ambapo kama watanzania , kwakushirikiana na viongozi wa dini kwa pamaoja
wanapaswa kusimama na kuliombea Taifa ili kuendelea kudumisha amani
iliyopo.
" Tangu nimezaliwa sijawahi kushuhudia vita, machafuko katika nchi
yetu, kikubwa huwa naona amani iliyotawala, Upendo, na umoja , sasa
nawasishi sana ndugu zangu tuendelee kuwa wamoja tusibaguane, kwa namna
yoyote ile , ili nchi yetu iendelee kuwa na amani" alisema Meya Mwita.
"Baba wataifa Hayati Mwalim Julius Nyerere enzi ya uhali wake
alikuwa akisisitiza sana kulinda amani ya nchi yetu, na sisi ambao tupo
hai hadi sasa , mambo ya vyama, Udini, Ukabila tuweke pembeni tusimame
kama Taifa moja.
Awali akijibu risala iliyoandaliwa na uongozi wa kanisa hilo, Meya
Mwita aliahidi kuchangia katika ujenzi huo mifuko 100 ya Simenti na
kiasi cha Fedha shilingi 500,000 huku aliwataka waumini wa kanisa hilo
kujitolea ili kufanikisha ujenzi huo.
Risala hiyo ilieleza kujenga kanisa la kisasa lenye uwezo wa
kuchukua waumini 600 ambapo jumla ya shilingi milioni 95 zinahitajika
ili kukamilisha ujenzi huo.
Px.
2Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam akisalimiana na waumini wa
kanisa hilo mara alipowasili katika viwanja vya kanisa la TAG lililopo
Kivule jijini hapa.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati
akifuatilia burudani zilizokuwa zikitumbuiza kwenye hafla hiyo. Wa
kwanza kulia ni mchungaji wa kanisa hilo Amosi Mbiga. Kushoto Mwenye
Shati jeupe aliyevaa tai ni Diwani wa kata ya Kivule Bonivenja Mollel.
Post a Comment