Rais wa TFF, Jamali Malinzi na wenzake
wataendelea kusota Lumande hadi Julai 17, 2017 bila kesi yao kutajwa,
kufuatia upande wa Jamhuri kushindwa kukamilisha upelezi wa kesi ya
uhujumu uchumi inayowakabili.
Wakili wa Serikali Nassoro Katuga mbele
ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri, leo Julai
3,2017 mahakamani hapo, alida kuwa Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika
na kuiomba Mahakama kupanga tarehe ya kutajwa kesi hiyo.
Ndipo Hakimu Mashauri aliipanga Tarehe 17 Julai mwaka huu, kuwa siku ya kutajwa kesi hiyo.
Jamali na Wenzake akiwemo Katibu Mkuu
wa TFF, Selestin Mwesigwa walitiwa mbaroni na Takukuru kwa tuhuma za
matumizi mabaya ya madaraka, na kufikishwa kizimbani leo Julai 3, 2017.
Post a Comment